Mujuru kuungana na MDC ili kumuondoa Mugabe

Joyce Mujuru
Image caption Joyce Mujuru

Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Joyce Mujuru anasema kuwa atafurahia kubuni muungano na chama cha upinzani cha MDC ili kumuondoa madarakani rais Robert Mugabe.

Bi Mujuru ameiambia BBC kwamba yuko tayari kufanya kazi na chama cha Movemnet for Democratic Change kinachoongozwa na Morgan Tsvangira na wengine kwa niaba ya raia wa taifa hilo.

Alizndua rasmi chama chake mapema mwaka huu baada ya kufutwa kazi kama makamu wa rais kabla ya kufukuzwa katika chama tawala cha ZANU PF .

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 92 amesema kuwa atawania muhula mwengine katika uchaguzi ujao.

Kumekuwa na maandamano katika wiki za hivi karibuni kuhusu hali mbaya ya kiuchumi nchini Zimbabwe.

Mada zinazohusiana