Bolt anyakua dhahabu mbio za mita 200 Olimpiki Rio

Usain Bolt Haki miliki ya picha Reuters

Mwanariadha Mjamaica Usain Bolt ameshinda mbio za mita 200 katika michuano ya Olympics huko Rio nchini Brazil na kujinyakulia medali ya dhahabu ya pili baada ya kunyakua ya michuano ya mbio za mita 100.

Ameshinda kwa kirahisi mbio hizo za mita 200 kwa kutumia sekunde 19.79. Bolt kwa sasa anahitaji kushinda mbio za mita 4x 100 za kupokezana vijiti ili kukamilisha medali ya tatu ya dhahabu kama alivyofanya katika michuano iliyopita.

Mapema wiki hii alidhihirisha kuwa ni mwamba wa mbio fupi pale aliposhinda mbio za mita 100 na kunyakuwa medali ya dhahabu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Usain Bolt akipiga picha na mashabiki

Katika matokeo mengine Marekani imenyakulia medali nyingine nne za dhahabu ikiwemo ya mwanariadha wake Ashton Eaton.