Rio: Mkenya Vivian Cheruiyot ashinda dhahabu

Taarifa hii haipatikani tena.
Rio: Mkenya Vivian Cheruiyot ashinda dhahabu

Mkenya Vivian Cheruiyot ameshinda dhahabu katika mbioa za mita 5000 za akina dada mjini Rio, na kuweka rekodi mpya ya mbio hizo kwa muda wa dakika 14 sekunde 26.17.

Nafasi ya pili nayo ilichukuliwa na mkenya mwanzake Hellen Obiri, ambaye alijishindia medali ya fedha kwa muda wa dakika 14 sekunde 29.77

Muithiopia Almaz Ayana ambaye alishinda dhahabu katika mbio za mita 10,000, alichukua nafasi ya tatu kwa muda wa dakika 14 sekunde 42.89.

Cheruiyot sasa amepata medali mbili baada ya kupata fedha katika mbio za mita 10,000.