Olimpiki Rio 2016: Matukio yaliyosisimua zaidi

Michezo ya Olimpiki Rio 2016 ilishuhudia matukio mengi ya kukumbukwa, baadhi mazuri na mengine mabaya. Haya hapa ni baadhi ya mambo yatakayokumbukwa sana.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mbeba bendera wa Tonga Pita Taufatofua alivutia wengi kwa mtindo wake wa mavazi sherehe ya ufunguzi.

Haki miliki ya picha @ragansmith

Picha moja iliyodhirisha tofauti katika kimo na unene ilikuwa hii ya mwanamichezo ya mazoezi ya viungo kutoka Marekani Ragan Smith na mchezaji mpira wa kikapu DeAndre Jordan.

Haki miliki ya picha Reuters

Kulikuwa pia na kisa cha urafiki licha ya uadui wa mataifa. Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Korea Kaskazini, wachezaji wawili wa mazoezi ya viungo ambao nchi zao ni mahasimu wakuu, walipiga picha pamoja.

Haki miliki ya picha NBC

Lakini hakukuwa na urafiki wakati wowote. Twitter 'iliwaka moto' baada ya bingwa wa uoegeleaji Michael Phelps kuonekana akimwangalia vibaya mpinzani wake Chad le Clos.

Haki miliki ya picha Reuters

Medali ya kwanza ya dhahau kwa wenyeji, iliyomwendea bingwa wa judo wa uzani wa kilo 57 Rafaela Silva, iliwapa kitulizo wakazi wa maeneo maskini Rio. Silva alizaliwa eneo maskini Rio na mwaka 2012 akatimuliwa mashindano London na kuelezwa kama "aibu kuu". Lakini mwaka huu ulikuwa wa fahari kwake.

Haki miliki ya picha Getty Images

Baada ya muda Phelps, mwogeleaji aliyeshinda medali nyingi, hatimaye alitabasamu baada ya kumshinda Clos wa Afrika Kusini fainali za 200m butterfly wanaume. Baadhi walipendekeza Clos alifaa kuangazia kuogelea badala ya kumwangalia mpinzani wake.

Haki miliki ya picha AP

Kulikuwa na mengine mazuri kando na ushindi. Rami Anis, mwogeleaji wa timu ya wakimbizi aliyetoroka Syria 2015 kwa boti na kupitia bahari ya Mediterranean hadi Uturuki alisifiwa sana baada ya kuandikisha muda wake bora zaidi 100m freestyle upande wa wanaume.

Haki miliki ya picha Getty Images

Si wanamichezo pekee waliovutia watu. Baadhi ya walinzi, waliopewa jukumu la kuwalinda waogeleaji maarufu, ambao walionekana kuzidiwa na upweke, waliwavutia watu pia.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kuna kumbukumbu pia kwa Fiji, ambao timu yao ya wachezaji saba wa kila upande waliimba na kushangilia kwa hisia baada ya kushinda fainali kwa kulaza Uingereza 34-7. Ilikuwa dhahabu ya kwanza kabisa kwa Fiji Olimpiki.

Haki miliki ya picha Getty Images

Nani atamsahau? Mwanamichezo wa mazoezi ya viungo kutoka Marekani Simone Biles, 19, alisismua kwa ustadi wake. Alishinda dhahabu nne na shaba.

Haki miliki ya picha Getty Images

Rangi ya maji katika kidimbwi cha Maria Lenk Aquatics Centre iligonga vichwa vya habari, ilipobadilika na kuwa kijani kibichi badala ya samawati. Baadaye ilibainika kwamba mabadiliko hayo yalitokana na viwango vya kemikali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mavazi? Picha za timu ya mpira wa wavu wa ufukweni kutoka Misri zilisambaa sana mtandaoni, baada ya Doaa Elghobashy kucheza akiwa amevalia hijab.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mwogeleaji Mmarekani Katie Ledecky alitawala, akivunja rekodi yake ya dunia kwa karibu sekunde mbili na kushinda fainali ya wanawake kuogelea 800m freestyle muda wake ukiwa dakika nane na sekunde 4.79. Alimaliza karibu sekunde 12 mbele ya wapinzani wengine.

Alishinda pia alishinda mashindao ya wanawake kuogelea 200m freestyle, t400m na kuogeleana kwa kupokezana 4x200m freestyle.

Haki miliki ya picha Getty Images

Rekodi ya kwanza ya dunia kuvunjwa uwanjani ilivunjwa na Muethiopia Almaz Ayana, ambaye alivunja rekodi ya awali kwa zaidi ya sekunde 14 na kushinda mbio za mita 10,000 wanawake.

Haki miliki ya picha AP

Raia wa Misri Islam El Shehaby alizua utata kwa kukataa kumsalimia mpinzani wake kutoka Israel Os Sasson baada ya kushindwa katika judo. El Shehaby alizomewa na mashabiki na baadaye akafukuzwa kutoka Rio.

Haki miliki ya picha Reuters

Mshindi wa dhahabu kutoka Singapor Joseph Schooling, aliyemuenzi sana Michael Phelps utotoni, alimshinda kuogelea 100m butterfly.

Haki miliki ya picha Reuters

Moja ya picha za kuvutia zaidi katika uendeshaji baiskeli ilipatikana wakati Laurine van Riessen, wa Uholanzi aliepusha ajali kati yake na Mfaransa Virginie Cueff kwa kuendesha baiskeli yake juu kwenye kizuizi.

Haki miliki ya picha EPA

Kusherehekea ushindi: Aurimas Didzbalis wa Lithuania alisherehekea kushinda shaba katika unyanyuaji uzani kitengo cha wanaume wa kilo 94.

Haki miliki ya picha Getty Images

Uingereza iliingiwa na wasiwasi alipotegwa na kuanguka, lakini Mo Farah aliamka na kuendelea na mbio na kutetea dhahabu yake mbio za mita 10,000. Ndiye Mwingereza wa kwanza kushinda dhahabu tatu Olimpiki michezo ya uwanjani.

Haki miliki ya picha BBC Sport

Si wote waliotokwa na machozi wakipokea nishani. Mwingereza Sir Bradley Wiggins badala yake aliuota ulimi wake nje baada ya kushinda dhahabu mashindano ya kuendesha baiskeli kama timu.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mpiga mbizi MchinaHe Zi alikuwa ameshinda fedha upigaji mbili kutoka kwa springboard 3m pale mwenzake Qin Kai alipojitokeza na kumchumbia. Alikubali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mkimbiaji kutoka Jamaica Usain Bolt naye hakuwa mchache wa vituko, alionyesha tabasamu akielekea kushinda nusufainali mita 100. Baadaye alishinda fainali akitumia sekunde 9.81.

Haki miliki ya picha Getty Images

Raia wa Afrika Kusini Wayde van Niekerk naye alivunja rekodi iliyodumu miaka 17, ambayo iliwekwa na Michael Johnson, kwa sekunde 0.15 na kushinda dhahabu mbio za mita 400. Mkufunzi wake ni nyanyake wa miaka 74.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kucheza nyoma? Mnyanyuaji uzani David Katoatau, kutoka Kiribati, alicheza ngoma kila alipofanikiwa kunyanyua uzaji. Alimaliza nambari sita kitengo cha uzani wa kilo 105.

Haki miliki ya picha Getty Images

Shaunae Miller wa Bahamas atakumbukwa kwa kupiga mbizi na kushinda dhahabu mbio za mita 400 wanawake.

Haki miliki ya picha EPA

Mwanbondia wa Ireland uzani wa Michael Conlan alishindwa kwa alama robo fainali na Mrusi Vladimir Nikitin. Conlan hakufurahishwa na uamuzi huo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ilikuwa ni furaha kwa wachumba wawili Waingereza. Laura Trott alishinda dhahabu mbili naye mchumba wake Jason Kenny akashinda dhahabu tatu. Wapenzi wawili, ambao wameshinda dhahabu 10 Olimpiki.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kunao waliotokwa na machozi, kwa sababu nyingine, kama Mfaransa huyu Renaud Lavillenie. Alitokwa na machozi baada ya kuzomewa na umati aliposhindwa na mwenyeji Thiago Braz da Silva fainali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kisa cha kushangaza zaidi Rio kilihusu madai ya wizi kutoka kwa washindi watatu wa dhahabu katika uogeleaji waliodai kwamba waliporwa katika kituo cha mafuta ya petroli. Baadaye ilibainika kwamba Wamarekani hao Ryan Lochte, Jimmy Feigen na Jack Conger walitunga madai hayo. Badala yake ndio walioharibu mali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Udugu? Ndugu, Alistair Brownlee na Jonny Brownlee ambao walishinda dhahabu na fedha katika triathlon walijibwaga chini kusherehekea ushindi.

Haki miliki ya picha AFP

Bolt, mara nyingine tena, alionyesha ucheshi wake, akimwelekezea kidole mwanariadha wa Andre De Grasse wakivuka mstari nusufainali ya 200m. Bolt alishinda katika fainali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Morolake Akinosun alimaliza mbio peke yake baada ya timu ya Marekani mbio za kupokezana vijiti 4x100m kuruhusiwa kurudia baada ya kupoteza kijiti. Waliendelea na kushinda fainali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Moyo wa Olimpiki ulijionyesha wazi Nikki Hamblin wa New Zealand (kushoto) na Abbey D"Agostino wa Marekani waliposaidiana kuinuka baada ya kugongana mbio za mita 5000 wanawake.

Haki miliki ya picha Getty Images

Refugee team at opening ceremony

Bolt akisherehekea baada ya kushinda nishani ya tisa Olimpiki. Alisema ushindi wa mbio za 100m, the 200m na 4x100m kupokezana vijiti ungemfanya "kutosahauliwa milele".

Haki miliki ya picha EPA

Brazil walifuta mkosi na machungu ya kulazwa 7-1 na Ujerumani nusufainali Kombe la Dunia kwa kulaza Ujerumani fainali Olimpiki. Neymar,

Haki miliki ya picha Getty Images

Mwingereza Mo Farah alishinda 5000m na 10000m na kuwa mtu wa pili, baada ya Lasse Viren wa Finland kutetea mataji hayo mawili Olimpiki.

Haki miliki ya picha Reuters

Na mwisho wa mashindano, ilikuwa shangwe sherehe ya kufunga michezo hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Haki miliki ya picha Patrick Smith

Mwenge wa Olimpiki ulizimwa kwa mvua bandia, kwenye usiku ambao mvua kubwa pia ilinyesha.

Haki miliki ya picha Reuters

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alionyesha watu kionjo cha michezo ijayo ya Tokyo 2020 kwa kutokea kwenye video akiwa amevalia kama mhusika wa michezo ya kompyuta Super Mario.

Haki miliki ya picha Reuters