Mtanzania aliyetukuka licha ya kumaliza mwisho Olimpiki
Huwezi kusikiliza tena

John Akhwari: Mtanzania aliyetukuka licha ya kumaliza mwisho Olimpiki

John Stephen Akhwari anakumbukwa duniani kote kwa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 1968 iliyofanyika nchini Mexico. Alijulikana kwa tukio la 'Nafasi ya Mwisho Iliyotukuka' katika mashindano ya Olimpiki.

Alikuwa ni mkimbiaji wa mwisho mbio za Marathon wakati wenzake wakiwa wamemaliza mbio hizo, lakini yeye pia hakukata tamaa licha ya kuumia na mguu wake kufungwa bendeji.

Mwandishi wetu Sammy Awami alimtembelea kijijini kwao Mbulu, Kaskazini mwa Tanzania na haya ndiyo mazungumzo yao.