Benteke hawezi kuwa 'Lionel Messi' Palace

Benteke Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Christian Benteke

Beki wa Crystal Place Damien Delaney amesema kumsajili Christian Benteke 'si Lionel Messi' na kwamba atahitaji kupokea usaidizi kutoka kwa wachezaji wengine katika klabu hiyo..

Benteke mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na The Eagles kutoka Liverpool kwa thamani ya pauni milioni 27.

'Hatumsajili Messi, ni (Benteke) mchezaji mzuri lakini si mchezaji ambaye anaweza kupata mpira na kubadilisha mchezo,'' Delaney aliambia gazeti la Evening Stardard.

Benteke huenda akajiunga na Crystal Palace wakikabiliana na Blackpool katika mechi ya EFL Jumanne.

'Benteke analeta uhali kwenye timu, kama mshambuliaji Connor Wickham. Ni wakati wetu kuacha kuzungumza sana na kuangazia ushindi," Dalaney aliongezea.