Wavuti wa Ethiopia wapuuza kutorejea nyumbani kwa Feyisa Lilela

Feyisa Lilela Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ethiopia ilishuka sana kwenye jedwa la viwango vya washindi wa Olyimpiki mwaka huu katika michezo ya Rio

Shirika la habari la taifa la Ethiopia -Fana Broadcasting Corporate limewashangaza wengi kwa kushindwa kutaja taarifa kuhusu mwana riadha wa nchi hiyo anaeomba uhamiaji Feyisa Lilela kwenye tovuti yake ya taarifa za kurejea kwa kikosi cha taifa kilichokua Brazil kwa michezo ya Olyimpiki.

Kikosi hicho kilipokelewa na maafisa wa serikali , alkiwemo Waziri wa Vijana na Michezo, Redwan Hussein, aktika uwanja kimataifa wa ndege wa Bole, iliripoti tovuti.

Feyisa alishenda medali ya shaba silver katika mbio za marathon, na alipo maliza mbio zake alikuja mikono yake kama ishara ya upinzani dhidi ya serikali kwa kuwakamata watu wa jamii ya Oromo, ambao ndio wanaounda kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia.

Ethiopia ilishuka sana kwenye jedwa la viwango vya washindi wa Olyimpiki mwaka huu katika michezo ya Rio vikilinganishwa na miaka michuano ya Olyimpiti sita iliyopita, lilibaini shirika la habari la kitaifa la Ethiopia Fana

Ilipata medali moja ya dhahabu, mbili za shaba na tano za fedha , ikichukua nafasi ya 44 katika jedwali la medali ambapo ilikua nambari tatu barani Afrika.