Januzaj aifungia Sunderland bao la kwanza

Adnan Januzaj Haki miliki ya picha PA
Image caption Adnan Januzaj

Adnan Januzaj ameifungia timu ya Sunderland bao lake la kwanza, na kuwasaidia kuichapa Shrewsbury kutoka Uingereza bao moja kwa nunge katika raundi ya pili ya Kombe la Ligi Uingereza.

Bao hilo limemsaidia meneja wa paka hao weusi David Moyes kupata ushindi wa kwanza tangu msimu huu kuanza.

Kiungo wa kati wa Sunderland Steven Pienaar, alipoteza nafasi nzuri katika kipindi cha kwanza na mshambuliaji Joel Asoro kijana mwenye umri wa miaka 17 akanusia lango la Shrewsbury mara mbili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Adnan Januzaj alifungia Manchester United bao lake la mwisho mwezi Agosti 2015

Shambuliaji wa Shrewsbury, Ivan Toney alijaribu kufunga bao lakini mlinda lango wa Sunderland Jordan Pickford alimnyima nafasi.

Haki miliki ya picha PA

Baada ya mechi hiyo klabu ya Sunderland imethibitisha difenda wa Atletico Madrid Javier Manquillo anapokea uchunguzi wa kiafya katika klabu hiyo.