Miamba wa Ulaya kufahamu wapinzani UEFA

Leicester City Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mabingwa wa ligi ya Uingereza, Leicester City

Leicester City, wanaoshiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza, watafahamu nani atakuwa mpinzani wao baadaye leo jioni droo itakapofanywa.

Droo itafanyika mwendo wa saa moja usiku saa za Afrika Mashariki siku ya Alhamisi.

Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich, Paris St- Germain na Juventus hawawezi kupangwa pamoja na mabingwa wa Uingereza, Leicester.

Arsenal, Tottenham, Manchester City pia hawataorodheshwa katika kundi moja na Leicester lakini katika ligi ya Scotland, Celtic wanaweza kuorodheshwa katika kundi moja nao.

Celtic walifuzu katika michuano ya makundi kwa kuichapa Israel, Hapoel Beer Sheva 5-4.

Klabu zilizo kwenye chungu kimoja haziwezi kuwekwa kwenye kundi moja.

Vyungu

Chungu 1: Real Madrid (Uhispania), Barcelona (Uhispania), Leicester City (Uingereza), Bayern Munich (Ujerumani), Juventus (Italia), Benfica (Ureno), Paris Saint-Germain (Ufaransa), CSKA Moscow (Urusi).

Chungu 2: Atletico Madrid (Uhispania), Borussia Dortmund (Ujerumani), Arsenal (Uingereza), Manchester City (Uingereza), Sevilla (Uhispania), Porto (Ureno), Napoli (Italia), Bayer Leverkusen (Ujerumani)

Chungu 3: Basel (Uswizi), Tottenham Hotspur (Uingereza), Dynamo Kiev (Ukraine), Lyon (Ufaransa), PSV Eindhoven (Uholanzi), Sporting Lisbon (Ureno), Club Brugge (Ubelgiji), Borussia Monchengladbach (Ujerumani)

Chungu 4: Celtic (Scotland), Dinamo Zagreb (Croatia), Monaco (Ufaransa), Besiktas (Uturuki), Legia Warsaw (Poland), Ludogorets Razgrad (Bulgaria), FC Copenhagen (Denmark), Rostov (Urusi)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Leicester hawawezi kupewa Barcelona au Real Madrid

Tarehe muhimu

  • 13-14 Septemba - Raundi ya kwanza ya mechi za makundi
  • 6-7 Desemba - Raundi ya Finali ya mechi za makundi
  • 14-15/21-22 Februari - Raundi ya 16, mechi ya mkondo wa kwanza
  • 07-08/14-15 Mechi - Raundi ya 16, mechi ya marudiano
  • 11-12 Aprili- Robo fainali, mechi za mkondo wa kwanza
  • 18-19 Aprili- Robo Fainali , mechi ya marudiano
  • 02-03 Mei - Robo Fainali, katika mechi ya mkondo wa kwanza
  • 09-10 Mei - Robo fainali, katika mechi ya marudiano
  • 03 Juni - Fainali (katika uwanja wa Cardiff)