Daniel Sturridge amlalamikia Jurgen Klopp

Daniel Sturridge Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Daniel Sturridge

Mchezaji wa Liverpool Daniel Sturridge amesema kocha wake Jurgen Klopp amekuwa akimchanganya kwa kumchezesha namba ambayo isiyo yake, na kudai kwamba yeye ni mshambuliaji wa pembeni na sio mshambuliaji wa kati.

Hayo yanajiri baada ya klopp kumchezesha Sturridge nafasi ya mshambuliaji wa kati katika baadhi ya mechi kiasi kwamba anashindwa kufanya vizuri na kumfanya kukosa furaha awapo uwanjani.

Daniel Sturridge amesema yeye anacheza kwa ajili ya timu na atacheza kwa ajili ya timu na si vinginevyo