Taifa Stars mpya kuivaa Nigeria mechi ya AFCON 2017

Wachezaji wa awali wa timu ya taifa ya Tanzania Haki miliki ya picha TFF
Image caption Wachezaji wa awali wa timu ya taifa ya Tanzania

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania 'Taifa Stars', Charles Boniface Mkwasa, ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.

Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali na Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.

Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa, Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Timu itaingia kambini Agosti 28, kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo huo.

Makipa

 • Deogratius Munishi - Young Africans
 • Aishi Manula - Azam FC

Mabeki

 • Kelvin Yondani - Young Africans
 • Vicent Andrew - Young Africans
 • Mwinyi Haji - Young Africans
 • Mohamed Hussein - Simba SC
 • Shomari Kapombe - Azam FC
 • David Mwantika - Azam FC

Viungo

 • Himid Mao - Azam FC
 • Shiza Kichuya - Simba SC
 • Ibrahim Jeba - Mtibwa Sugar
 • Jonas Mkude - Simba SC
 • Muzamiru Yassin - Simba SC
 • Juma Mahadhi - Young Africans
 • Farid Mussa Tenerif ya Uhispania

Washambuliaji

 • Simon Msuva - Young Africans
 • Jamal Mnyate - Simba SC
 • Ibrahim Ajib - Simba SC

John Bocco - Azam FC

Mbwana Samatta - KRC Genk ya Ubelgiji.