Polisi Brazil wamemshtaki muogeleaji wa Marekani Ryan Lotche

Uhalifu huo hukumu yake ni miezi nane jela
Image caption Uhalifu huo hukumu yake ni miezi nane jela

Polisi nchini Brazil wamemshtaki muogeleaji wa olympic wa marekani Ryan Lotche kwa kutoa madai ya uongo kuwa yeye na wenzake watatu waliibiwa kwa kushikiwa bunduki wakati wa michuano ya Rio kitu amabacho ni upotoshaji.

Uhalifu huo hukumu yake ni miezi nane jela.

Msemaji wa polisi ameeleza kuwa kesi hiyo imepelekwa mahakamani na Lotche atatakiwa kujibu mashtaka hayo. Idara ya marekani imesema inatambua ombi hilo.

Lotche ameondoka Brazil kabla hajahojiwa na polisi. Ameomba msamaha kwa kusema uongo juu ya kuibiwa. Lotche amepoteza wadhamini wake wakubwa wanne kufuatia tukio hilo na hivyo kuweka hatarini kazi yake ya uogeleaji

Image caption Kesi hiyo imepelekwa mahakamani na Lotche atatakiwa kujibu mashtaka hayo