Klabu ya Ufaransa yamtaka Mario Balotelli

Mario Balotelli Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mario Balotelli

Klabu ya Nice nchini Ufaransa imeeleza nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli.

Mchezaji huyo wa miaka 26 amechezea Liverpool mechi 28, na akawafungia mabao manne tangu anunuliwe na aliyekuwa mkufunzi wa Liverpool Brendan ambaye alimtoa AC Milan kwa £16m mwaka 2014.

Mshambuliaji huyo ameambiwa na meneja wa sasa Jurgen Klopp kwamba anaweza kutafuta klabu mpya.

Kufikia sasa hakuna mkataba uliotiwa saini baina ya Nice na Liverpool, lakini Balotelli hakuhudhuria mazoezi ya wachezaji wa Liverpool eneo la Melwood Alhamisi.

Balotelli, ambaye pia amefanya mazungumzo na klabu ya FC Sion ya Uswizi alikaa AC Milan kwa mkopo msimu uliopita ambapo aliwafungia bao moja Serie A.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii