Barcelona kumsajili Paco Alcacer kutoka Valencia

Paco Alcacer
Image caption Paco Alcacer

Klabu ya Barcelona imetangaza rasmi kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Paco Alcacer kutoka Valencia kwa mkataba wa miaka mitano.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye aliondolewa katika kikosi cha Valencia kilichoshinda bao 1-0 dhidi ya Eibar Jumamosi iliyopita, alifanyiwa vipimo vya afya Barcelona Jana kabla ya kukamilisha uhamisho wake huo uliogharimu euro milioni 30.

Alcacer amefunga mabao 43 katika mechi 124 alizoichezea Valencia huku akiitwa mara 13 kukichezea kikosi chake cha timu ya taifa.

Akihojiwa Alcacer amesema pamoja na kuwa anaondoka Valencia lakini siku zote itakuwa ni klabu ya moyo wake na kuwashukuru mashabiki kwa kipindi chote walichomuunga mkono