Siku ya mwisho sokoni: Wachezaji 10 wa kufuatilia

Mamadou Sakho, Samir Nasri, Saido Berahino & Lamine Kone Haki miliki ya picha Getty Images

Kipindi cha kuhama wachezaji Uingereza kitamalizika saa saba usiku saa za Afrika Mashariki Jumatano na tayari pilka pilka za ununuzi wa mwisho zimeanza.

Hawa hapa ni wachezaji ambao unafaa kuwafuatilia kwa makini?

1. Jack Wilshere (Arsenal)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jack Wilshere alichezea Gunners mechi tatu pekee msimu uliopita

Wilshere hajawekwa kikosi cha England kitakachokabili Sweden na ana muda wa kuangazia mustakabali wake. Meneja Arsenal Arsene Wenger hatarajiwi amruhusu mchezaji huyo wa miaka 24 aondoke kwa mkataba wa kudumu. Ana kipaji ilhali anahitaji kucheza mechi zaidi kuweza kujinoa makali, fursa ambayo hawezi kupata Arsenal kwa sasa. Hivyo, huenda akatumwa nje kwa mkopo.

Anaweza kuelekea: Valencia, Roma, Juventus, West Ham United, Crystal Palace, Southampton, Middlesbrough.

2. Moussa Sissoko (Newcastle United)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Newcastle wanataka £35m akumwachilia Sissoko

Moussa Sissoko, 27, alicheza vizuri sana Euro 2016 na kuwasaidia kufika fainali ambapo walishindwa na Ureno. Klabu yake kwa sasa inacheza ligi ya daraja la pili, Championship na hatarajiwi kukaa huko. Lakini anayetaka kumnunua lazima atoe £35m.

Anatafutwa na: Juventus, Inter Milan, Everton, Spurs, Crystal Palace, West Bromwich Albion.

3. Saido Berahino (West Bromwich Albion)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Tony Pulis alisema Saido Berahino ataruhusiwa kuondoka pesa nyingi "zikiwekwa mezani"

Berahino atasalia West Brom au ataondoka?

Mchezaji huyo wa miaka 23 alionekana kukaribia kuondoka West Brom, baada yake kuandika miezi 12 iliyopita kwenye Twitter kwamba hangecheza tena baada yake kushindwa kuhamia Tottenham.

Kwa mara nyingine tena, kunaonekana kuwa na uwezekano kwamba huenda ataondoka baada yake kuchezeshwa kama nguvu mpya mechi dhidi ya Middlesbrough Jumapili.

Anaweza kwenda wapi: Stoke City, Crystal Palace.

4. Lamine Kone (Sunderland)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Lamine Kone anatafutwa na Everton

Meneja wa Sunderland David Moyes binafsi alizuia ofa ya £18m kutoka kwa Everton waliotaka kumchukua Lamine Kone. Lakini Everton bado wanamtaka na raia huyo wa Ivory Coast anaonekana kutaka kuondoka.

Chelsea ni klabu inayomtafuta bei na huenda wakamtafuta.

Anaweza kwenda wapi: Everton, Chelsea.

5. James McCarthy (Everton)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption McCarthy ameambia Everton anataka kuondoka

Meneja wa Everton Ronald Koeman amesisitiza kwamba beki huyo wa miaka 25 kutoka Jamhuri ya Ireland hauzwi lakini kuna uvumi kwamba huenda akaondoka Goodison Park kukitokea mtu wa kulipa £20m.

Anaweza kuhamia wapi: Crystal Palace, Sunderland, Newcastle United, Leicester City.

6. Wilfried Bony (Manchester City)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Meneja wa West Ham Slaven Bilic anamtaka Wilfried Bony

Mshambuliaji huyu wa miaka 27 kutoka Ivory Coast hajafana Manchester City ambako alihamia baada ya kununuliwa £28m kutoka Swansea City Januari 2015.

Ni wazi kwamba Bony hayumo kwenye mipango ya meneja mpya Pep Guardiola.

Anaweza kwenda wapi: Stoke City, West Ham United, Everton.

7. Mario Balotelli (Liverpool)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Mario Balotelli alinunuliwa kutoka AC Milan £16m mwaka 2014

Mario Balotelli ameshindwa kufana tangu anunuliwe na Liverpool £16m kutoka AC Milan Agosti 2014. Amewafungia mabao manne pekee katika mechi 28 ambazo amewachezea.

Msimu uliopita alitumwa AC Milan kwa mkopo.

Nice wa Ligue 1 wanamtafuta lakini Palermo wa Italia pia wamekuwa wakimtafuta.

Anaweza kuhamia wapi: Nice, Palermo.

8. Samir Nasri

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nasri huenda akafurahia kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iwapo atajiunga na Sevilla

Nasri ni mchezaji mwingine ambaye inaonekana hatasalia Etihad chini ya Pep Guardiola.

Mchezaji huyo wa miaka 29 alianza akiwa kwenye benchi mechi dhidi ya West Ham Jumapili ambayo walishinda 3-1.

Nasri amekuwa akitafutwa na mabngwa watetezi wa Europa League Sevilla wa Uhispania pamoja na Besiktas wa Uturuki.

Anaweza kwenda: Sevilla, Besiktas.

9. Islam Slimani (Sporting Lisbon)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Slimani amekuwa Sporting tangu 2013

Slimani, 28, raia wa Algeria, alionekana kuwaaga mashabiki Sporting Lisbon baada ya kutokwa na machozi akiondoka uwanjani mechi dhidi ya Porto wikendi.

Amekuwa akitafutwa na Leicester.

Slimani, ambaye ni mshambuliaji, amefunga mabao 33 katika mechi 44 alizochezea Sporting tangu mwanzo wa msimu uliopita.

Anakadiriwa kuwa na thamani ya karibu £35m.

Anaweza kwenda: Leicester City.

10. Mamadou Sakho (Liverpool)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Stoke City wanamtaka beki Mamadou Sakho kwa mkopo

Sakho amehangaika Liverpool na meneja Jurgen Klopp amemwambia anaweza kuondoka kwa mkopo.

Sakho, 26, tayari amekataa kuhamia Stoke City na West Brom, lakini Liverpool wamekuwa wakisisitiza aondoke ndipo apate nafasi ya kucheza mechi zaidi. Hivyo, nani ajuaye? Huenda akaondoka siku ya mwisho.

Anaweza kwenda: West Brom, Stoke City.