Joe Hart asajiliwa na Torino ya Italia

Aliyekuwa kuwa kipa wa Manchester City asajiliwa na Torino ya Italia
Image caption Aliyekuwa kipa wa Manchester City asajiliwa na Torino ya Italia

Klabu ya Italy ya Torino imemsajili kipa wa Manchester City Joe Hart kwa mkopo wa muda wa msimu uliosalia.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lilimpatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ruhusa kuondoka kambi ya Uingereza siku ya Jumatatu ili aweze kuelekea Italy kwa ukaguzi wa kimatibabu.

''Usajili wa Joe Hart ni furaha kubwa '',ilisema taarifa kutoka kwa mtando wa klabu hiyo ya Serie A.

Hart huenda akaanza katika mechi ya Torino dhidi ya Atlanta mnamo tarehe 11 mwezi Septemba