Wilfried Bonny ajiunga na Stoke City kwa mkopo

Wlifried Bonny ajiunga na Stoke City kwa mkopo
Image caption Wlifried Bonny ajiunga na Stoke City kwa mkopo

Klabu ya Stoke City imemsajili mshambuliaji Wilfried Bony kwa mkopo kutoka Manchester City.

Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 27,ameanzishwa mara 15 tangu ajiunge na City kwa kitita cha pauni milioni 28 kutoka Swansea mnamo mwezi Januari 2015 , lakini hajacheza chini ya mkufunzi mpya Pep Guardiola.

Stoke pia imemsajili kipa wa Derby, Lee Grant mwenye umri wa miaka 33 kwa mkopo hadi mwezi Januari.

Wakati huohuo Beki wa Porto na Uholanzi Bruno Martins Indi mwenye umri wa miaka 24 anaendelea na mazungumzo ya kusajiliwa na klabu hiyo.