Manchester City yakata rufaa dhidi ya Aguero

Sergio Aguero
Image caption Sergio Aguero

Klabu ya Manchester City imekata rufaa dhidi ya shtaka la kucheza vibaya linalomkabili mshambuliaji wake Sergio Aguero dhidi ya mchezaji Winston Reid kutoka West Ham.

Aguero alimpiga kiwiko Winston Reid

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28,alizozana na Reid wakati wa ushindi wa 3-1 katika mechi ya ligi ya Uingereza.

Iwapo atapatikana na hatia ,mchezaji huyo wa Argentina atapigwa marufuku ya mechi tatu na kukosa deby ya Manchester mnamo tarehe 10 mwezi Septemba.

Pia ataikosa mechi ya ligi dhidi ya Bournemouth pamoja na ile ya kombe la EFL dhidi ya Swansea.