Yaya Toure awachwa nje ya kikosi cha vilabu bingwa

Pep Guradiola na Yaya Toure
Image caption Pep Guradiola na Yaya Toure

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amemwacha nje kiungo wa kati wa timu hiyo yaya Toure katika kikosi chake cha kombe la vilabu bingwa Ulaya mwaka 2016-17.

City haikuweza kuweka zaidi ya wachezaji 17 wa kigeni katika kikosi chao.

Na Guradiola ana wachezaji 18 licha ya kuwauza wachezaji wanne wa kigeni kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho.

Vilabu vinaweza kubadilisha wachezaji watatu baada ya mechi za kimakundi lakini Toure mwenye umri wa miaka 33 hatocheza dhidi ya Borussia Monchengladbach ,Celtic na Barcelona.

Mchezaji huyo wa timu ya Ivory Coast alishiriki pakubwa katika ushindi wa klabu hiyo tangu anunuliwe kutoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 24 mwaka 2010.

Alichezeshwa mara moja msimu huu,katika awamu ya pili ya kombe la vilabu bingwa dhidi ya Steaua Bucharest,wakati City ilipokuwa ikiongoza 5-0 katika mechi ya kwanza.