Sergio Aguero kukosa mechi dhidi ya Manchester United

Sergio Aguerro
Image caption Sergio Aguerro

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero atakosa mechi ya debi kati ya timu yake na Manchester United mnamo tarehe 10, Septemba baada ya kupigwa marufuku kwa mechi tatu.

Kikao cha shirikisho la soka nchini Uingereza kilimpata na hatia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa kucheza vibaya baada ya kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji wa West Ham Winston Reid katika ushindi wa City wa 3-1 Jumapili iliopita.

Aguero anayeichezea Argentina pia hatoshiriki katika mechi za Manchester City dhidi ya Bournemouth mnamo tarehe 17 Septemba pamoja na ile ya kombe la raundi ya tatu la EFL dhidi ya Swansea mnamo tarehe 21 mwezi Septemba.

Image caption Sergio Aguerro

Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu msimu huu na City ambao wako juu ya jedwali kwa kushinda mecho zote walizocheza.