Rooney aandika rekodi mpya kucheza michezo England

Rekodi hii inaipita ile ya David Beckham ya michezo 115
Image caption Rekodi hii inaipita ile ya David Beckham ya michezo 115

Wayne Rooney ameandika historia ya kuwa mchezaji aliyeichezea timu ya taifa ya England mara nyingi zaidi, kwa wachezaji wa ndani ya uwanja.

Ulikuwa mchezo wake wa 116 kuiwakilisha England alipocheza na Slovakia katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2018.

Rekodi hii inaipita ile ya David Beckham ambaye aliichezea timu ya Taifa la England mechi 115.

Image caption Rooney akipokea maelekezo wakati wa mchezo

Mlinda mlango Peter Shilton, ndiye anaishika rekodi ya jumla kwa kuichezea England mara 125.