Kell Brook kuzipiga na Gennady Golovkin

Bingwa wa uzani wa Kati Genady Golovkin na mpinzani wake Kell Brook kutoka Uingereza Haki miliki ya picha AP
Image caption Bingwa wa uzani wa Kati Genady Golovkin na mpinzani wake Kell Brook kutoka Uingereza

Bondia wa Uingereza Kell Brook analenga kufuata nyayo za Sugar Ray Leonard wakati atakapokabiliana na mfalme wa uzani wa kati Gennady Golovkin mjini London siku ya Jumamosi.

Brook,ambaye ndio bingwa wa uzani wa Welter anaruka mizani miwili ili kukabiliana na Golovkin ambaye ameshinda mapigano yake yote kwa njia ya Knockout.

Bingwa wa zamani wa uzani wa Welter duniani Sugar Ray Leonard alirudi katika ulingo wa masumbwi mwaka 1987 baada ya kustaafu na kumshinda bingwa wa uzani wa kati wakati huo Marvin Hagler.

Image caption Kell Brooks kulia akizipiga

''Nataka kufanya kile ambacho Leonard alifanya na Hagler,nitatumia kasi na miguu yangu kumkabili Golovkin, alisema Brooks.

''Ninamuogopa kwa kweli.Najua ni mrushaji wa makonde mazito na ndio sababu hakuna mtu anayetaka kupigana naye.Lakini hofu hiyo inanipa motisha kwa sababu itanifanya niwe mwangalifu zaidi na kuwa kama paka''.