Shangwe Uganda kufurahia kufuzu AFCON 2017

Shangwe Uganda kufurahia kufuzu AFCON 2017

Sherehe zimekuwa zikiendelea kote nchini Uganda kufuatia timu ya taifa ya nchi hiyo kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika baada ya kusubiri kwa kipindi cha karibu miaka 40.

Mara ya mwisho Uganda ilicheza Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1978.

Wamefuzu tena baada ya kuishinda Comoro 1-0 mjini Kampala. Omar Mutasa alikuwepo na ana maelezo zaidi.