Tyson Fury kuzipiga tena na Klitschko

Tyson Fury kushoto akimenyana na Wladmir Klitschko katika pigano lao la kwanza
Image caption Tyson Fury kushoto akimenyana na Wladmir Klitschko katika pigano lao la kwanza

Pigano la marudiano kati ya bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury's dhidi ya Wladmir Klitscko limethibitishwa kufanyika Octoba 29.

Bingwa wa Uingereza Fury mwenye umri wa miaka 28 alijishindia mataji ya WBO,WBA, na IBF kutoka kwa raia huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 40 mnamo mwezi Novemba mwaka 2015,lakini akajiondoa katika pigano la marudio lililopangwa kufanyika mwezi Julai kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.

Pigano hilo litafanyika katika ukumbi wa Manchester.

''Ninafurahi kwamba tutapigana tena.sasa tutalenga kuwapatia mashabiki kile walichokitaka'',alisema meneja wa Tyson Fury na mjombake Peter.

Klitschko alikuwa hajawahi kushindwa kwa miaka 11 na alimiliki mikanda hiyo tangu mwaka 2006 kabla ya kupoteza kwa Fury mjini Dusseldorf kwa wingi wa pointi.