Marcus Rashford afunga hat-trick

Marcus Rashford Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Marcus Rashford

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford amelifungia hat-trick taifa lake katika mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 dhidi ya Norway.

Tayari mchezaji huyo ameifungia klabu yake katika mechi yake ya kwanza katika ligi ya Uingereza na ile ya Ulaya.

Rushford mwenye umri wa miaka 18 alifunga kwa umbali wa maguu 18 kabnla ya kuongeza bao la pili na kufunga mkwaju wa penalti katika bao lake la tatu.

Nathaniel Chalobah,Ruben Loftus-Cheek na Lewis pia walifunga.

Ushindi huo wa rahisi unamaanisha kwamba timu hiyo chini ya ukufunzi wa Gareth Southgate iko pointi mbili juu ya Switzerland katika kilele cha kundi hilo,huku ikiwa imesalia na mechi mbili mojawapo ikiwa ni ile dhidi ya wapinzani wao wa karibu.

Norway ambayo ilishinda 4-1 kupitia kichwa cha Ghayas Zahid inasalia kuwa ya tatu.