Rais wa kamati ya kimataifa ya Olympic, kuchunguzwa

Olimpic
Image caption Thomas Bach Rais wa kamati ya Olimpic

Polisi nchini Brazil wamesema kuwa wanahitaji kuongea na Rais wa kamati ya kimataifa ya Olympic, Thomas Bach, kuhusu kuhusika na mpango haramu wa kuuza tiketi kwenye michuano ya Rio iliyokamilika mwezi uliopita, ambapo polisi wamesema watamhoji kama shahidi, na si mtuhumiwa.

Maofisa walipata barua pepe kutoka kwa bwana Bash kwenda kwa mmoja wa maofisa wa kamati hiyo bwana Patrick Hickley, ambaye alikamatwa mwezi uliopita mjini Rio na anakabiliwa na mashitaka.

Hickley amekanusha kuhusika na mpango wowote wa kuuza tiketi za Olimpiki. Pia bwana Thomas Bach hajarudi Rio tangu kumalizika kwa michuano ya Olympic na amekosa ufunguzi wa sherehe za Paralympic zilizofanyika siku ya jumatano.