Angelique Kerber ndio mshindi wa US Open

Angelique kerber
Image caption Angelique kerber

Angelique Kerber wa Ujerumani ameshinda tuzo la mchezo wa tenisi upande wa wanawake katika mashindano ya US Open jijini New York.

Alimshinda Karolina Pliskova wa Czech Republic, aliyekuwa akicheza kwa mara ya kwanza katika shindano hilo la Grand Slam mwaka huu baada ya kushinda lile la Australia Open mnamo Januari.

Siku ya Jumapili bingwa wa mchezo huo upande wa wanaume, Novack Jokovich, atatetea taji lake dhidi ya Stan Wawrinka wa Switzerland.