Algeria yadaiwa 'kususia' mechi dhidi ya Israel

Timu ya Algeria ya mchezo wa Goalball yadaiwa kususia mechi dhidi ya Israel
Image caption Timu ya Algeria ya mchezo wa Goalball yadaiwa kususia mechi dhidi ya Israel

Kamati kuu ya kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu inachunguza kwa nini timu ya mpira wa goalball ya Algeria ilishindwa kuwasili jijini Rio ili kushiriki katika mashindano na Marekani na Israel.

Hadi kufikia sasa wanachama saba wa timu hiyo hawajawasili, kwa madai kuwa walikabiliwa na matatizo ya usafiri.

Lakini kuna madai kuwa timu ya Algeria ilitaka kususia mechi hiyo dhidi ya Israel kwa sababu ya uhasama wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.

Goalball ni mchezo wa wasioona ambapo mpira unaochezwa unafungiwa kengele.

Timu ya Algeria ilitazamiwa kupambana na Marekani Ijumaa na kisha Israel Jumamosi.