Barcelona yalazwa nyumbani na timu iliopanda daraja

Mchezaji wa Alavez akisheherekea ushindi wa klabu hiyo dhidi ya Barcelona
Image caption Mchezaji wa Alavez akisheherekea ushindi wa klabu hiyo dhidi ya Barcelona

Klabu ya Barcelona ilishangazwa iliposhindwa nyumbani na klabu iliopanda daraja ya Alavez huku mkufunzi Luis Enrique akiwaacha nje Lionel Messi na Luis Suarez.

Mashambuliaji wa Brazil Deyverson aliwanyamazisha mashabiki wa Nou Camp wakati alipofunga krosi ya Kiko Femenia akiwa maguu saba karibu na goli.

Beki Jenermy Mathieu alisawawazisha kupitia bao zuri la kichwa kutokana na kona iliopigwa na Neymar.

Ibai Gomez hatahivyo alifunga bao la ushindi ,akimfunga kipa Jasper Cillesen ndani ya boksi mda mfupi tu baada ya Lionel Messi kuingia kwa mabingwa hao wa La Liga.

Suarez aliingizwa baada ya bao la Gomez lakini Alavez ilijikakamua na kupata ushindi wake wa kwanza katika uwanja wa Nou Camp tangu mwaka 2000.

Barca sasa wako pointi tatu nyuma ya viongozi Real Madrid ambao waliicharaza Osasuna 5-2 siku ya Jumamosi ikiwa ni mechi ya kwanza ya Ronaldo tangu apate jeraha.