Paralimpiki yavunja rekodi ya mauzo ya fedha nyingi

Kuongezeka kwa mauzo kumetokana na bei nafuu na matangazo
Image caption Kuongezeka kwa mauzo kumetokana na bei nafuu na matangazo

Mauzo ya tiketi katika michezo ya walemavu ya paralimpiki yamefikia milioni 1.8 hivi sasa, mauzo hayo yamefanya michezo hii kuwa ya pili kwa mahudhurio makubwa katika historia.

Mwishoni mwa wiki watu wengi walinunua katika kituo cha michezo hiyo,si zaidi ya wiki mbili baada ya waandaji kutangaza kupunguza bei kwasababu ya hali mbaya ya kiuchumi iliyosababishwa na mauzo mabaya ya tiketi.

Kuongezeka kwa mauzo kumetokana na bei nafuu na matangazo.

Image caption Mojawapo ya viungo bandia vya wachezaji

Paralympik ya London ya mwaka 2012 ndio inayoongoza kwa mauzo ya tiketi ya karibu milioni 2 na nusu.