Stan Wawrinka atwaa ubingwa US OPEN 2016

Wawrinka ni mchezaji mwenye umri mkubwa kushinda US Open tokea Ken Rosewall aliposhinda 1970
Image caption Wawrinka ni mchezaji mwenye umri mkubwa kushinda US Open tokea Ken Rosewall aliposhinda 1970

Mswitzerland Stan Wawrinka amefanikiwa kuchukua ubingwa wa US Open kwa mara ya kwanza baada ya kushinda mchezo wa fainali kwa seti 6-7 1-7 6-4 7-5 6-3 dhidi ya bingwa mtetezi wa michuano hiyo Mserbia Novak Djokovic.

Wawrinka,31 anayeshikilia ubora namba tatu duniani amemfunga Djokovic ambaye ni namba moja kwa ubora duniani na kwa sasa Wawrinka ameshinda jumla ya Grand slam 3 huku akiwa hajashinda taji la Wimbledon.

Image caption Wawrinka amechuana na Djokovic mara 24 na kushinda mara tano pekee