Balotelli asema anajutia sana kujiunga na Liverpool

Balotelli Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mario Balotelli kwa sasa anachezea Nice ya Ufaransa

Mshambuliaji wa Nice Mario Balotelli amesema kujiunga na Liverpool, 'ulikuwa uamuzi mbaya zaidi aliowahi kuufanya maishani mwake.'

Mwitaliano huyo alifunga mabao manne katika mechi 28 alizochezea Liverpool baada ya kujiunga nao kutoka AC Milan mwaka 2014 kwa thamani ya dola milioni 16.

''Isipokuwa mashabiki, ambao hunishabikia, na wachezaji kadhaa ambao tunasikilizana, sipendi klabu yenyewe," Balotelli ameiambia runinga ya Ufaransa ya Canal Plus.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Balotelli akifunga bao la kwanza katika klabu ya Nice

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alisema hayo kabla ya kufunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza na klabu ya Nice katika michuano ya Ligue 1 walipofunga mabao 3-2 dhidi ya Marseille siku ya Jumapili.

Meneja Brendan Rodgers, aliyemsajili Balotelli, alipigwa kalamu na Liverpool mwezi Oktoba mwaka 2015, na Jurgen Klopp akachukua hatamu.