Paralimpiki: Mwanariadha mlemavu Tamiru apinga serikali ya Ethiopia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tamiru Demisse aonyesha alama ya upizani kwa serikali ya Ethiopia

Mwanariadha wa Ethiopia anayeshiriki katika michezo ya walemavu ya paralimpiki, Tamiru Demisse alionyesha ishara za kupinga serikali alipokuwa akikamilisha mbio zake mjini Rio, Brazil.

Tamiru alimaliza katika nafasi ya pili katika mita 1500 T13 mashindano ya watu wenye ulemavu wa kuona.

Ishara hiyo ni sawa na ile ya mwanariadha wa Ethiopia na mshindi wa medali ya fedha wa mbio za marathon za Olimpiki Feyisa Lilesa.

Lilesa alifanya ishara hiyo alipokamilisha mbio zake za marathon.

Alama hiyo ni ishara kutoka kwa wandamanaji kutoka jamii ya Oromo nchini Ethiopia ambao wamekuwa wakiandamana kwa miezi kadhaa wakitaka haki zao ziheshimiwe.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Feyisa Lilesa

Feyisa kwa hivi sasa yuko Marekani, baada ya kusema itakuwa hatari kwake kurudi nchini Ethiopia.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii