John Terry kutocheza wiki moja Chelsea

John Terry Haki miliki ya picha Getty Images

Nahodha wa klabu ya Chelsea ya Uingereza John Terry atakaa nje kwa takriban siku 10 baada ya kuumia akicheza dhidi ya Swansea Jumapili.

Mchezaji huyo aliumia kano za mguuni wakati wa mechi hiyo ambayo walitoka sare 2-2.

Terry, 35, atakosa mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Liverpool Ijumaa na pia mechi ya Kombe la EFL ugenini Leicester Septemba 20.

Wachezaji wapya David Luiz au Marcos Alonso huenda wakajaza nafasi yake wakati atakapokuwa hawezi kucheza.