Arsene Wenger: 'Upendo' kwa Arsenal ulinifanya niwakatae Paris St-Germain

Arsene Wenger Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger aliongoza Arsenal kushinda Ligi ya Premia 1997-98, 2001-02 na 2003-04

Meneja wa Arsene Wenger amesema "upendo" wake kwa klabu ya Arsenal ulimfanya kukataa kujiunga na Paris St-Germain ya Ufaransa.

PSG watakuwa wenyeji wa The Gunners hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne jioni.

Wenger, 66, anaadhimisha kuongoza Arsenal kwa miaka 20 mwezi ujao.

Mkataba wake katika klabu hiyo unamalizika majira ya joto 2017.

Kwa mujibu wa L'Equipe, PSG walimtafuta 2011, 2013 na 2014.

Alipoulizwa ni kwa nini akakataa kujiunga na PSG, Wenger alisema "Simesalia Arsenal muda huo wote kwa sababu ni klabu yenye sifa nizipendazo - na hiyo ndiyo sababu.

Arsenal wameshinda mataji matatu ya ligi na vikombe sita vya FA chini ya Wenger.

Hata hivyo, hawajashinda ligi tangu msimu wa 2003-04 na baadhi ya mashabiki wamemtaka aondoke.