Ligi ya mabingwa Ulaya UEFA yaanza kwa kishindo

Mlinda mlango wa Arsenal, Ospina alikuwa kikwazo kwa PSG
Image caption Mlinda mlango wa Arsenal, Ospina alikuwa kikwazo kwa PSG

Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya imeanza usiku wa kuamkia leo, ambapo jumla ya michezo saba kwenye makundi matano ilipigwa kwenye viwanja tofauti. Kundi A Basel ya nchini Uswiz ilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.

PSG ikiwa nyumbani ililazimiswa sare ya bao 1-1 dhidi ya washika bunduki wa London Arsenal, huku PSG wakitangulia kupata goli la mapema mnamo sekunde ya 30 ya mchezo kupitia mshambuliaji wake Edinson Cavani huku Goli la kusawazisha kwa upande wa Arsenal likifungwa na Alexis Sanchez kwenye dk ya 78.

Image caption Alexis Sanchez akiifungia goli Arsenal

Tukio kubwa katika mchezo huo ni kadi mbili nyekundu zilizotolewa kwa timu zote mbili, Olivier Geroud akipewa kadi nyekundu kwenye dk ya 90 ya mchezo baada ya kadi ya njano aliyopewa kwenye dk ya 88, huku kwa upande wa PSG Marco Verratti nae pia akiambulia kadi nyekudu kwenye dakika hiyo hiyo ya 90 baada ya kadi ya njano aliyopewa kwenye dk ya 8.

Image caption Wachezaji wa Barcelona wakishangilia ushindi

Lakini matokeo makubwa yalikuwa huko Barcelona baada ya kuibamiza Celtic kwa idadi ya magoli 7-0 huku messi akianza na hat- trick, magoli mengine yalifungwa na Suarez ambaye alipachika magoli mawili, Neymar na Iniesta wakipata goli moja moja, huku Mousa Dembele akikosa mkwaju wa Penalti kwa upande wa Celtic

Mchezo mwingine wa kundi D Bayern Munich ilicharanga FC Rostov ya nchini Urusi Magoli 5-0 huku Atletico Madrid ya nchini Hispania ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya mwenyeji wake PSV Eindhoven ya nchini uholanzi

Matokeo mengine

Benfica1 - 1 Besiktas

Dynamo Kyiv 1 - 2 SSC Napoli