Rais akaribia kupatikana Uchaguzi wa UEFA

Ceferin ana karibu waungaji mkono 40 wa awali kutoka nchi 55
Image caption Ceferin ana karibu waungaji mkono 40 wa awali kutoka nchi 55

Mkuu wa chama cha soka cha Slovenia, Aleksander Ceferin yuko mbioni kushinda uchaguzi wa Urais wa chama cha soka barani Ulaya UEFA katika uchaguzi utakao fanyika Athens nchini Ugiriki.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vya Ceferin vimeiambia BBC kuwa ana karibu waungaji mkono 40 wa awali kutoka nchi 55 wanachama wa UEFA.

Image caption Mpinzani wake mkuu ni Mdachi Michael van Praag

Mpinzani wake mkuu ni Mdachi Michael van Praag ambaye ni mwanachama wa kamati ya utendaji na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi.

Aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo ambaye yupo kizuizini kwa sasa kwa madai ya kukiuka sheria za maadili Michel Platini anajiandaa kuhutubia kabla ya uchaguzi baada ya kupata ruhusa maalum ya kutoa hutuba fupi kutoka bara za la maadili la UEFA.

Image caption Aleksander Ceferin

Mfaransa huyo alizuiliwa kujihusisha na soka kwa muda wa miaka minne baada ya kugundulika kuwa amepokea karibu Euro milioni 1.6 malipo yaliyoidhinishwa na aliyekuwa Rais wa uefa Sepp Blatter mwaka 2011.