EUROPA yatimua vumbi, Man U yalala ugenini

Mlinzi wa Feyenoord Eric Botteghin alikuwa nyota wa mchezo
Image caption Mlinzi wa Feyenoord Eric Botteghin alikuwa nyota wa mchezo

Michuano ya UEFA ndogo au EUROPA imeanza katika hatua ya makundi, mechi 24 zimechezwa ambapo Manchester United ikiwa ugenini ilipokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi.

Na klabu ya Genk ya ubelgiji anayochezea Mbwana samata pia ikiwa ugenini imepokea kichapo cha magoli 3-2 dhidi ya Rapid Wien ya Austria.

Image caption Man U walipiga shuti 8 kati ya 18 za Feyenoord

Mbwana Samata alitolewa kwenye Dk ya 78 na nafasi yake kuchukuliwa na Nikos Karelis.

Matokeo mengine

AZ Alkmaar 1 Dundalk 1

Southampton 3 Sparta Prague 0

FK Qarabag 2 Slovan Liberec 2

Sassuolo 3 Ath Bilbao 0

Viktoria Plzen 1 Roma 1

Astra Giurgiu 2 FK Austria Vienna 3

M'bi Tel-Aviv 3 Zenit St P 4

Apoel Nic 2 FC Astana 1

BSC Young Boys 0 Olympiakos 1

FSV Mainz 05 1 Saint-√Čtienne 1