Andy Murray kupambana na Juan del Potro Devis Cup

Andy Murray
Image caption Andy Murray

Andy Murray ambaye anashikilia namba mbili kwa ubora duniani atacheza na aliyekuwa bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani Juan Martin del Potro ikiwa ni mchezo kwanza wa kombe la Devis katika hatua ya nusu fainali utakao pigwa mjini Glasgow Scotland leo saa 13:00 mchana.

Del Potro ambaye yupo nafasi ya 64 kwa ubora duniani na amerejea kutoka majeruhi.

Alipoteza pambano dhidi ya Murry kwenye michuano ya olimpic mjini Rio mwezi uliopita.

Image caption Davis Cup linachukuliwa kuwa ndilo kombe la dunia la tennis

Lakini pia ndugu wawili Andy na Jamie Murray watacheza pamoja siku ya jumamosi katika mchezo wa pamoja wakiiwakilisha timu ya Uingereza.

Davis Cup linachukuliwa kuwa ndilo kombe la dunia la tennis ambalo husimamiwa na shirikisho la tennis la dunia ITF.