Guardiola: ''Ni Messi pekee anayemshinda Kevin de Bryne''

Kevin de Bryne kushoto na Lionel Messi Kulia wakichezea mataifa yao
Image caption Kevin de Bryne kushoto na Lionel Messi Kulia wakichezea mataifa yao

Mkufunzi wa Klabu ya Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa anamthamini mchezaji wake Kevin de Bryne kuwa katika kiwango cha juu kama mchezaji mwengine yeyote yule isopokuwa Lionel Messi wa Barcelona.

Raia huyo wa Ubelgiji aliifungia City bao la Kwanza katika ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Bournemouth siku ya Jumamosi.

Kwa sasa mchezaji huyo ana magoli 18 na usaidi wa pasi 16 katika mechi 48 alizochezea The Blues ambao wameanza msimu huu kuweka rekodi ya mechi nane bila kushindwa katika michuano yote.

Guardiola: Messi ni mchezaji wa kiwango cha kivyake.Hakuna anayemfika baada yake Kevin anamfuata.

Katika kipindi cha kazi yake Guardiola amefanikiwa kuwafunza wachezaji bora dunia akiowemo,Xavi na Andres Iniesta akiwa Barcelona na Arjen Robben na Thomas Muller akiwa Bayern Munich.