Faili za mwanariadha wa Burundi zadukuliwa

Francine Niyonsaba
Image caption Francine Niyonsaba

Mwanariadha wa Burundi ambaye alishinda medali ya fedha katika mbio za mita 800 upande wa wanawake katika michezo ya Olimpiki mjini Rio ni Mwafrika wa kwanza ambaye faili zake za kimatibabu zilidukuliwa na wadukuzi wa mtandao wa Fancy Bears.

Fancy Bear ni jina la wahalifu wa mtandaoni ambao waliiba habari za kibinafsi za wanariadha ambazo zinamilikiwa na shirika la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli WADA na wanaangazia utumizi wa dawa za kusisimua misuli zilizopigwa marufuku.

Dawa ambayo Francine Nyonsaba aliruhusiwa kutumia na shirikisho la riadha duniani IAAF ni Tibolone.

Dawa hiyo hutumika kuongeza homoni za kike katika wanawake ambao wana homoni za kike chache.