Guardiola amtaka Yaya Toure aombe msamaha au asicheze tena

Mkufunzi Pep Guradiola na kiungo wa kati Yaya Toure
Image caption Mkufunzi Pep Guradiola na kiungo wa kati Yaya Toure

Meneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa hatomchezesha tena Yaya Toure hadi atakapoomba msamaha kwa klabu hiyo na wachezaji wenzake kutokana na matamshi ya ajenti wake.

Toure mwenye umri wa miaka 33 ameichezea City mara moja msimu huu na aliwachwa nje katika kikosi cha vilabu bingwa Ulaya.

Ajenti wake Dimitri Seluk amesema kuwa kiungo huyo wa kati ''alifedheheshwa'' na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda kinyang'anyiro hicho.

Guardiola:''lazima aombe msamaha la sivyo hatocheza''.

Raia huyo wa Uhispania pia anataka msamaha kutoka kwa Seluk.

Alisema kuwa ni uamuzi mgumu kumwacha nje Toure katika kikosi cha kombe la Vilabu bingwa Ulaya.

''Iwapo ana tatizo anafaa kuzungumza wenzake katika klabu ,alisema Gurdiola,ambaye alikuwa mkufunzi wa Barcelona wakati Toure alipouzwa kwa Manchester City 2010.