Wakala wa Yaya Toure akataa masharti ya Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Manchester City Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amejipata katika vita vya maneno na wakala wa kiungo wa kati Yaya Toure baada ya kukosa kumteua kiungo huyo katika kikosi cha wachezaji 25 watakaoshiriki katika mechi za klabu bigwa barani Ulaya katika hatua ya makundi.

Guardiola amesema hatamteua mchezaji huyo hadi pale wakala wake Dimitry Seluk, atakapoomba msamaha kwa matamshi aliyotamka kwa vyombo vya habari.

Lakini ajenti huyo amesema katu hatafanya hivyo na badala yake akasisitiza kwamba meneja huyo ndiye afaaye kuomba radhi.

''Kwa nini ni muombe msamaha Guardiola? Sijui maneno ninayostahili kutamka kuomba radhi, kwa sababu sijafanya kitu chochote. Iwapo nitajihisi kuomba radhi, basi nitaomba radhi hiyo, lakini sihisi kufanya hivyo. Kile Guardiola anachokitaka hakitawezekana,'' alisema Seluk kwenye runinga ya Sky Sport News.

Amesema meneja huyo amewakosea watu wengi akigusia mtangulizi wake Manuel Pellegrini na kisha kipa nambari moja wa Manchester City Joe Hart ambaye alilazimika kuondoka klabu hiyo majira ya joto baada ya kuachwa nje ya mipango ya Guardiola.

"Ni lazima awaombe radhi Yaya na Hart na Pellegrini. Guardiola anashinda mechi kadha na kuanza kufikiria kwamba yeye ni mfalme."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa kati Yaya Toure

Seluk amesema mteja wake, Toure ,33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.

Guardiola amesema iwapo Seluk atamuomba msamaha yeye, klabu hiyo na wachezaji wa timu hiyo hapo ndio Yaya atakuwa na nafasi sawa ya kushiriki katika michezo yote.

''Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kweye kikosi," Guardiola ameongezea.

Guardiol alikuwa kocha wmkuu Barcelona Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii