Serengeti Boys kuelekea Rwanda Alhamisi

Timu ya vijana ya Serengeti Boys kutoka Tanzania
Image caption Timu ya vijana ya Serengeti Boys kutoka Tanzania

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, nchini Tanzania Serengeti Boys inatarajia kuondoka kesho Alhamisi kuelekea Rwanda, kuweka kambi ya muda mfupi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Congo Brazzaville utakaochezwa Oktoba 2, mwaka huu.

Serengeti ipo katika hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika Madagascar, mwakani kufuatia kubakiwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Congo ambayo katika mchezo wa awali waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 .

Ofisa habari wa shirikisho la soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema, awali benchi la ufundi lilipendekeza kambi iwe Madagascar lakini TFF imeonelea ni vyema waelekee Rwanda ambapo ni karibu zaidi .

Serengeti itakuwa huko hadi muda wa kwenda nchini Congo utakapofika na wataondokea hukohuko.