Mayweather avunja pigano na nyota wa UFC

Conor Mc Gregor na Mayweather
Image caption Conor Mc Gregor na Mayweather

Bondia mstaafu Floyd Mayweather amesema kuwa pigano kati yake na mpiganaji Conor Mc Gregor halitofanyika.

Bingwa huyo wa zamani wa mizani mitano tofauti ,mwenye umri wa miaka 39 alisema mapema mwaka huu kwamba angependa kupigana na nyota huyo wa Ireland.

''Nilijaribu kuona pigano hilo linafanyika,lakini hatukuweza kwa hivyo tunasonga mbele''.Mayweather aliambia FightHype.com.

''Nafurahia kuwa na heshima kubwa katika masumbwi na wala sipigani tena''.

McGregor awali alikuwa amesema kuwa alivutiwa na pigano hilo ,lakini ilitarajiwa kuwa Mayweather angetafuta kiasi cha fedha anazotaka ili pigano hilo lifanyike.