Man United kukutana na Man City kombe la ligi

Manchester United kumenyana na wapinzani wao wa Jadi Man City ugani Old Trafford Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United kumenyana na wapinzani wao wa Jadi Man City ugani Old Trafford

Klabu ya Manchester United na Manchester City watakutana katika roundi ya nne katika kombe la Ligi ya Uingereza (EPL) uwanjaini Old Trafford.

United waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Northampton siku ya Jumatano huku City wakiibuka na mabao mawili kwa moja dhidi ya Swansea.

Kwengineko, timu ya West Ham itawakaribisha mahasimu wa Uingereza Chelsea, huku Tottenham wakielekea Liverpool.

Timu zitakazo toka sare zitacheza kuanzia tarehe 24 mwezi Oktoba.

City walishinda kombe hilo msimu uliopita baada ya kuishinda Liverpool kwa mikwaju ya penalti.

United wakiongozwa na Jose Mourinho wamepata ushindi mara tatu mfululizo dhidi ya Northampton.

DROO KAMILI:

West Ham dhidi ya Chelsea

Manchester United dhidi ya Manchester City

Arsenal dhidi ya Reading

Liverpool dhidi ya Tottenham

Bristol City dhidi ya Hull

Leeds dhidi ya Norwich

Newcastle dhidi ya Preston

Southampton dhidi ya Sunderland