Ranieri: Mgogoro kati yangu na Mourinho umekwisha

Mkufunzi wa Leicester Claudio Ranieri
Image caption Mkufunzi wa Leicester Claudio Ranieri

Mkufunzi wa Leicester Claudio Ranieri anasema kuwa Jose Mourinho ni ''mtu mzuri'' na kwamba mgogoro wowote uliokuwepo kati yao umepitwa na wakati.

Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza wanachuana na Klabu ya Manchester United siku ya Jumamosi huku wakufunzi hao wawili wakiwahi kuzozana hapo awali.

Mourinho alimuita Ranieri ''mtu anayeshindwa'' baada ya kumrithi kama mkufunzi katika klabu ya Chelsea na pia akamtusi alipokuwa mkufunzi wa Intermilan.

Image caption Mkufunzi wa Manchester United Claudio Ranieri

Ranieri alisema: Mourinho ni mkufunzi mzuri ,mwerevu na mwenye kutumia akili .

Maswala yaliosababisha mzozano ni ya zamani.

" Mkufunzi huyo wa Manchester United alishinda mataji matatu na Inter Milan mwishoni mwa ukufunzi wake wa miaka mitatu 2010,huku Ranieri akiwa mkufunzi wa Juventus na Roma katika kipindi hicho hicho.