Je Giggs amezea mate kuwa meneja wa Swansea?

Ryan Giggs Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Giggs, aliihama M U kama meneja msaidizi tangu July - na kumaliza uhusiano wake wa miaka 29 na klabu hiyo.

Ryan Giggs huenda anapendelea kuwa meneja wa klabu ya Swansea ikiwa kiongozi wa sasa Francesco Guidolin ataachia ngazi kama tetesi zinavyobashiri.

Giggs, mwenye umri wa 42, aliihama Manchester United kama meneja msaidizi tangu July - na kumaliza uhusiano wake wa miaka 29 na klabu hiyo.

Swansea tayari imepata pointi 4 kutoka kwa mechi 5 walizocheza msimu huu lakini inasemekana klabu hiyo ya Wales ina mpango wa kubadili uongozi.

Sio kwamba Giggs ndio chaguo pekee la Swansea iwapo mabadiliko hayo yatafanyika.

Isitoshe, tangu alivyoondoka Old Trafford , Giggs amekuwa akiendeleza zaidi biashara zake za siku nyingi kwenye maswala ya matangazo ya biashara ya TV work na pia katika Salford City, klabu ambayo anaimiliki pamoja na watimu wenzake wa zamani Paul Scholes, Nicky Butt, Gary na Phil.

Awali Giggs alionesha hamu ya kumrithi Louis van Gaal kama meneja wa Manchester United lakini naibu mwenyekiti Ed Woodward badala yake akamchagua Jose Mourinho baada ya kumfuta kazi Louis van Gaal hapo Mei.