Conte: Nahitaji mda kuiboresha Chelsea

Meneja wa Chelsea Antonio Conte mwenye umri wa miaka 47 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Chelsea Conte aliwahi kushinda vikombe vitatu vya ligi alipokuwa na Juventus huko Italy

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema anahitaji mda kuimarisha timu yake Chelsea kucheza anavyotaka yeye ili ipate matokeo bora, Je mashabiki watamuelewa?

''The Blues'' kama wanavyoitwa walikwenda sare na Swansea, wakapoteza mechi yao na Liverpool kabla kufanikiwa kuigonga Leicester City 4-2 kwenye mechi zao za hivi majuzi.

"Ni kawaida wakati unaanza kazi kwenye timu mpya unahitaji mda kutekeleza kile unachokusudia, nami naahidi tutaiboresha Chelsea'' Conte amenukuliwa kusema

Chelsea wanakutana na mahasimu Arsenal Jumamosi huku meneja wa Gunners Arsene Wenger akiwa anatafuta ushindi wa kusherehekea vizuri miaka 20, ifikapo 1 October, tangu kuwasimamia Wana-Emirates hao.

Kibarua cha Conte hata hivyo si rahisi- Msimu wa ligi uliopita Chelsea walibugia magoli 53.

"Hii inamaanisha lazima tufanye kazi ya ziada timu nzima tuboreshe upande wa ulinzi wetu, kwani iwapo unataka kuwa bingwa kisawasawa dawa ni kutofungwa mabao mengi hivyo."

Katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Arsenal itabidi Conte atafute dawa ya dharura kwani hatakuwa na mchezaji anaemtegemea sana John Terry ambae anauguza jeraha.