Pambano la Tyson dhidi ya Klitschko laahirishwa

Pambano lilitarajiwa Octoba 29 Haki miliki ya picha Getty Images

Bingwa wa masumbwi uzani mzito kutoka Uingereza Tyson Fury ameahirisha maregeo ya pambano lake na Wladimir Klitschko kwa mara ya pili kwasababu ''afya yake hairidhishi''.

Mapromota wake hawakufichua taarifa zaidi lakini wamesema " hali yake ni mbaya mno na haimruhusu kushiriki pambano hilo".

Fury, mwenye umri wa miaka 28, alimshinda Klitschko kutoka Ukraine kwa pointi katika pambano la kwanza mnamo Novemba mwaka jana.

Regeleo la pambano la awali lilipangwa Julai 9 katika uwanja wa Manchester Arena, na liliahirishwa hadi Juni baada ya Fury kuvunja fupa la kisigino chake.

Pambano jipya la maregeo kati ya mabondia hayo wawili liliangwa kufanyika Octoba 29.

"Tyson sasa inabidi fanayiwe matibabu anayohitaji ili aweze kupona kikamilifu," Hennessey Sports iliongeza.

"Tunaomba radhi kwa wote wanaohusika katika pambano hili na mashabiki wote wa masumbwi waliotazamia maregeo hayo. Ni wazi kuwa Tyson pia amehuzunishwa na hali ilivyo.

"Tutatoa taarifa zaidi katika muda unaofaa."